PICHA

PICHA

Breaking News

MAFUTA 5 YA NYWELE YA KUJARIBU KWA MA-NATURALISTA


Hey Loves, wale ma-naturalista hii inawahusu sana. Kama una natural hair unatakiwa kujua ni mafuta gani ya kutumia ili nywele zako zikuwe vizuri, zi-shine, ziwe nzito..na all this inategemea na products unazotumia katika nywele zako. Starting from mafuta, shampoo, conditioner na mazagazaga mengine mengi..leo hii nawaletea mafuata ambayo unatakiwa ujaribu kwa your natural hair ili uweze kujua which one among these yatafaa nywele zako..as you know kila mtu ana nywele tofauti.


Haya Ndio Mafuta Ya Kujaribu Katika Natursl Hair::
1.JOJOBA OIL.

  • Jojoba oil yana the same molecular structure na yale mafuta ambayo yanatengenezwa na ngozi ya kichwa chako mwenyewe(scalp)..hivyo yanakubalika na kichwa. A lot of women wenye natural hair huwa wanayatumia haya sana.
  • Unaweza kutumia jojoba oil kuchanganya kwenye your home made deep conditioner au hata hair mask..ingia HAPAkujua jinsi ya kutengeneza.
  • Jojoba oil yenyewe unaweza kuyatumia as a moisturizer, yanalainisha nywele na kuepusha nywele zisikakamae.
  • Yanarejesha nywele zilizo haribika kutokana na heat kwa wale mnao piga pasi/kunyoosha natural hair zenu..na unaweza ukayapaka kila siku kwasababu ni mepesi.


2.CASTOR OIL.

  • Castor oil yana natural anti-bacterial, vitamin E na protein kwa wingi ambayo inasaidia kukuza nywele zilizo katika na kuepusha nywele kukatika..so kama una shed sana nywele jaribu haya.
  • Inasaidia kuondoa mba kichwani na kuponya vidonda vya fungus kichwani, chukua mafuta haya na uwe una massage polepole kichwani.
  • Inasaidia kukuza nywele mara 3 haraka kuliko uotaji wa kawaida, wengi wanayotumia haya wanasema kuwa nywele zao zimekuwa haraka sana.

*Unaweza mix Jojoba na Castor oil ukapaka kwa pamoja for better results.
Ingia HAPA kusoma benefits zingine za Castor oil.



3.COCONUT OIL.

  • A lot of naturalistas wanatumia sana coconut oil, yana low molecular weight na hivyo usiljai kuhusu nywele zako kuzidi mafuta, unaweza paka kila siku.
  • Yana-moisturize na hydrate nywele, ukipaka yana saidia kuvuta unyevu na kuzipa nywela maji ili zisikakamae..hivyo ni mazuri kwa wale wenye nywele kavu.
  • Unaweza kutumia kama conditioner, ukisha osha nywele zako unapaka haya. Unatumia pia kukuza nywele, kuondoa mba.


4.AVOCADO OIL.

  • Haya yana nutrients nyingi, kama vile Vitamin A,B,D&E, Protein, Iron, Magnesium ambazo husaidia kukuza nywele pia.
  • Yana saidia nywele zilizokatika, yanalainisha na kung'arisha nywele na hata kuzilinda against the sun..yani ni kama SPF.
  • Unaweza ukayachanganya na shampoo ukiwa unaosha nywele zako, au hata kwenye deep treatment utakayotengeneza.


5.OLIVE OIL.

  • Haya ni great sealant kama coconut oil, yani yanasaidia ku-trap maji/unyevu kwenye nywele zako ili zisikauke na kukakamaa.
  • Pia yanasaidia kwa wale wenye mba.
  • Yanafaa kwa wale wenye sensitive skin, sio rahisi kupata allergic reaction.
  • Unaweza kuongezea olive oil katika conditioner yako ili upate better results.

Hakuna maoni