PICHA

PICHA

Breaking News

SAMBUSA: MAPISHI

MAPISHI YA SAMBUSA ZA NYAMA / JINSI YA KUPIKA SAMBUSA ZA NYAMA HATUA KWA HATUA .
Ndugu wapenzi, Leo tunakuja na Jinsi ya kupika Sambusa Za nyama. Sambusa Hupendwa na wengihasa za nyama. Sambusa ni Tamu sana, wengi hupenda kula pamoja na Juisi, soda na hata chai.
Mapishi ya Sambusa Za Nyama /Jinsi ya kupika sambusa hatua kwa hatua
Mahitaji


½ kilo Nyama ya iliyosagwa
kijiko 1 kikubwa cha chakula cha Pilipili manga
Kijiko kimoja cha chakula cha kitunguu Thomu na tangawizi iliyosagwa
Mafuta ya kupikia Kiasi
Vijiko vinne unga ngano au ute wa yai kwa kufungia sambusa
Kaki za sambusa/manda/ chapati nyepesi (unaweza kununua zilizokuwa tayari zimeshakatwa kwa ajili ya sambusa au kama utanunua zile sheet pana utazikata kwa inchi 4 upana wa ruler yaani upate mistari 3
Directions
Kausha nyama ya kusaga kwa kiyunguu swaumu (thomu) na tangawizi pamoja na chumvi mpaka ikauke vizuri Iwache ipoe.
Kata kata majani ya kotmiri weka upande Kata kata upate vipande vidogo vidogo(chop) vya vitunguu maji.
Zikate pili pili zako slice za mviringo vidogo vidogo.
Wakati ukimaliza matayarisho haya na nyama yako itakuwa ishapoa kabisa hapo ndio utachanganya,bizari nzima pamoja na pilipili manga pamoja na vitu vyote ulivyokwisha vitayarisha
Koroga unga ndani ya kibakuli au ute wa yai
Weka kaki kwa mfungo wa triangle yaani pembe tatu kama kofia na
weka mchanganyiko wa nyama yako kiasi na uanze kuzifunga sambusa zako na ukifika mwisho hapo ndipo upake unga wako kwa ajili ya kuifunga isifunguke wakati wa kuchoma, pendelea kutumia kaki 2 kwa kila sambusa moja.
Kuchoma kwake ikiwa unazifanya na kuzichovya hapo hapo mafuta lazima yawe baridi (ninakusudia uweke mafuta na uzitie sambusa kabla hayajapata moto).
Na ikiwa uliziweka kwenye friji zikaganda basi unatakiwa uzichome kwa mafuta ya moto
Muhimu


Watu wengi hupata usumbufu katika kufunga sambusa, Jaribu mara kwa mara utafanikiwa tu, ni kiasi cha kuzowesha mikono kufuatisha ile Triangle tu.
Pia waweza kutupia njegere kiasi zilizopikwa katika mchanganyiko wako wa nyama ili kupendezesha zaidi. Kama nilivyofanya katika sambusa zangu hapo juu.
JINSI YA KUTENGENEZA MANDA (SAMOSA PASTRY)
Mahitaji:-
🔸Unga wa ngano vikombe 4
🔸Chumvi 1/2 kjk chai
🔸Mafuta vjk 4 chakula
🔸Maji vikombe viwili kasoro
🔸Mafuta kwa ajili ya kupaka
🔸Unga kunyunyiza


MAELEKEZO:-
1.Changanya mahitaji yote kisha kanda kufanya unga mlaini kwa muda wa dk 10. Funika acha ukae kwa dk 15.
2.Gawa unga wako vipande kumi na mbili kisha tengeneza viduara
3. Sukuma viduara kimoja baada ya kingine kufanya chapati ndogo ndogo kisha chukua chapati moja weka chini paka mafuta kisha nyunyiza unga na sambaza vzr,weka chapati ya pili juu yake utaendelea kw utaratibu hui kubebanisha chapati sita sita.
4. Chukua chapati sita ulizobebanisha,zibinye mwisho kuzibana vizuri kisha sukuma kufanya chapati moja kubwa.Rudia kwa za pili
5. Choma katika moto mdogo kabisa hadi ipate kuiva ila isibadili rangi wala isikauke na usikaangie mafuta kama chapati just unaibabua tu.
6. Kata manda zako mara nne.Hakikisha unazifunika na kitambaa safi zisikauke zikipoa hifadhi katika mfuko wa plastic.
Manda tayari kututumika kwa kufungia sambusa na rolls.
Hivyo ndivyo Jinsi ya kupika Sambusa za nyama. Ahsanteni

Maoni 1 :

  1. Napenda sana sambusa za nyama na umenisaidia kuongeza ujuzi wa upikaji wa sambuza za nyama nimekuwa nikitumia njia tofauti tofauti kupika sambuza za nyama mfano: https://www.bongolives.com/2018/01/jinsi-ya-kupika-sambusa-za-nyama.html

    JibuFuta